Home Habari za michezo ISHU YA KUPULIZIA DAWA KWENYE VYUMBA VYA WACHEZAJI…MASAU BWIRE AFUNGUKA KUKUTANA NA...

ISHU YA KUPULIZIA DAWA KWENYE VYUMBA VYA WACHEZAJI…MASAU BWIRE AFUNGUKA KUKUTANA NA HALI HIYO…AITAJA TIMU…


Msemaji wa Klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire, amesimulia jinsi alivyowahi kupuliziwa dawa akiwa katika vyumba vya uwanja hali iliyopelekea kulazwa hospitalini

Akizungumza katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao (Zoom) na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa michezo Bwire amesema mara nyingi suala hilo limekuwa likichukuliwa kama utani ila linaathiri wachezaji wengi

“Mwaka 2014 iliniathiri pale Stand, Shinyanga, tulipata adha hii na mimi nililazwa, na wapo watu walikuja wakatusihi tuendelee kucheza, lakini baadae ikaonekana ni uvumi, kitu ambacho kinafanya kuwafanya wale wanaofanya kuendelea kufanya hivyo”

Masau Bwire ameitaka serikali pamoja na mamlaka za kusimamia soka kufuatilia kwa karibu masuala ya wachezaji kupuliziwa dawa za kupunguza nguvu viwanjani kwa kuwa yapo kweli na sio uvumi

SOMA NA HII  BAADA YA MUDATHIR YAHAYA...JEMBE LINGINE LINALOTUA YANGA HILI HAPA....NABI ABARIKI....