Home Uncategorized GLOBAL FC KUMALIZANA NA DSJ FC MAZIMA LEO

GLOBAL FC KUMALIZANA NA DSJ FC MAZIMA LEO


MATAJIRI wa Sinza, timu ya Global FC, leo Ijumaa wanatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji cha Dar es Salaam (DSJ) kwenye Uwanja wa Boom, Ilala Bungoni jijini Dar.
Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kuwa wa upinzani mkali kutokana na baadhi ya wachezaji wa Global FC kuwahi kusoma katika chuo hicho.
Akizungumza na Championi Ijumaa, mchezaji wa Global FC ambaye aliwahi kuwa Rais wa chuo hicho, Lunyamadzo Mlyuka alisema: “Hatutakubali kufungwa na wadogo zetu, kama watatufunga basi itakuwa ni fedheha kubwa sana, hivyo tutajitahidi kushinda japokuwa mpira una matokeo ya kikatili,” alisema mchezaji huyo.

 Katika mechi iliyopita, Global FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kill Veterani.
SOMA NA HII  KIPCHONGE MAMBO MAGUMU ASHINDWA KUTETEA TAJI LAKE KISA MAUMIVU YA NYONGA