Home Uncategorized KILA BAADA YA DAKIKA 90 YANGA INAFUNGWA BAO MOJA NA INAFUNGA BAO...

KILA BAADA YA DAKIKA 90 YANGA INAFUNGWA BAO MOJA NA INAFUNGA BAO MOJA NDANI YA VPL


MWENDO wa Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara unashtua kutokana na mzani wake kuwa sawa pande zote mbili kwa upande wa kufunga na kufungwa mabao ndani ya ligi.
Yanga iliyo chini ya Luc Eymael, imefunga jumla ya mabao 15 na imefungwa jumla ya mabao 15 kwenye mechi 15 ilizocheza ambazo ni sawa na dakika 1,350. Yanga ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 90 na inafungwa bao moja kila baada ya dakika 90.
Kwenye mabao hayo 15 ambayo wamefunga Yanga, kinara wa kutupia ni David Molinga ambaye ametupia mabao matano, Patrik Sibomana ametupia manne, Mrisho Ngassa ana bao moja na asisti moja,Abdulaziz Makame , Yikpe, Mapinduzi Balama , Mohamed Issa ‘Mo Banka’ na Niyonzima hawa wametupia mojamoja.
Kinara wa kutupia pasi za mwisho ndani ya Yanga kwa sasa ni Deus Kaseke ambaye ana jumla ya pasi tatu alizotoa huku Yanga ikiwa imejikusanyia pointi 28 kibindoni.
Juma Abdul, nahodha msaidizi na beki ndani ya Yanga amesema kuwa wanazidi kupambana ili kuzuia idadi ya mabao ya kufungwa kwani ni kitu ambacho kinamkasirisha Kocha Mkuu, Luc Eymael.
SOMA NA HII  HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOSAFIRI KUELEKEA BOTSWANA