Home CAF WASOMALI WATAJA KILICHOWAKWAMISHA BONGO

WASOMALI WATAJA KILICHOWAKWAMISHA BONGO


KOCHA Mkuu wa Horseed FC ya Somalia amesema kuwa wachezaji wake walijitahidi kusaka ushindi ila ilikuwa ngumu kutokana na upinzani mkubwa kutoka kwa Azam FC.

Horseed FC katika mchezo wa jana wa Kombe la Shirikisho mbele ya Azam FC ilipaswa kushinda mabao zaidi ya matatu kwa kuwa mchezo wa awali ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 na jana ilikubali kuona ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Horseed FC 0-1 Azam FC.

  Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Horseed FC, Mohamed Hussein Ahmed amesema kuwa walikuja na mbinu mpya ya kupata ushindi ila ilishindikana kutojana na wachezaji wake kukosa umakini katika kumalizia nafasi za mwisho.

“Wachezaji walikuwa na kazi kubwa ninawapongeza kwa kuwa hawajaruhusu mabao mengi ila ile hali ya kushinda ilikosekana.

“Unajua ukiwa unacheza na timu ambayo inawachezaji wenye ushindani mkubwa basi kila mmoja anahitaji kupata matokeo na ikishindikana tunasema ni sehemu ya mchezo.

“Nawapongeza wachezaji wamefanya kazi kubwa wanahitaji pongezi ni wakati wetu wa kuangalia pale ambapo tumekosea ili tuweze kufanya vizuri wakati ujao,” amesema.

SOMA NA HII  REFA MECHI YA SIMBA SC VS HOROYA AC...KAMA YUPO FEA FEA VILEE...MNYAMA ASHINDWE YEYE KWA MKAPA