Home CAF KOMBE LA SHIRIKISHO KUFUTWA… RAIS CAF “SIKUWEKA PESA MAKUSUDI…AMEFUNGUKA HAYA

KOMBE LA SHIRIKISHO KUFUTWA… RAIS CAF “SIKUWEKA PESA MAKUSUDI…AMEFUNGUKA HAYA

KOMBE LA SHIRIKISHO KUFUTWA... RAIS CAF

Ishu ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), kutazamiwa kuyafuta mashindano yake ya pili kwa ukubwa ya Kombe la Shirikisho, kulingana na ripoti zilizopo, inaonekana kuzua mijadala kwa sasa katika mitandao ya kijamii.

Kombe la Shirikisho Afrika ambalo lilianzishwa 2004 kutokana na kuunganishwa kwa Kombe la CAF na Kombe la Washindi muda wowote linaweza kutangazwa kufutwa kama alivyosema rais wa CAF, Patrice Motsepe mwanzoni mwa mwaka huu kule Ivory Coast wakati wa fainali za mataifa ya Afrika.

Motsepe alisema, “Tunaweza kufuta Kombe la Shirikisho. Tuna mashindano mengi sana. Hatuwezi na hatutakuwa na mashindano mengi….Ligi ya Mabingwa ni bora; tunataka kuilinda na kuikuza.

Ndio maana sikuweka kwa makusudi pesa za AFL kuwa zaidi ya Ligi ya Mabingwa. Sikutaka kujenga dhana kwamba, AFL iko juu ya Ligi ya Mabingwa.”

Kauli hiyo kwa sasa inatafsiriwa kwamba mchakato huo umeiva hivyo klabu za Tanzania, Simba, Yanga, Azam na nyinginezo ambazo
zinapigania nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao wanatakiwa kuwa tayari na hili.

Kufutwa kwa Kombe la Shirikisho Afrika kuna maana kuwa michuano ya kimataifa katika ngazi ya klabu itasalia miwili, Ligi ya Mabingwa Afrika na AFL.

Itakuwaje sasa? Kwa mujibu wa taarifa inaelezwa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itachukua nafasi ya Kombe la Shirikisho la CAF kama shindano la pili la klabu barani Afrika.

Mshindi wa African Footabll League sasa ataliwakilisha bara katika Kombe la Dunia la klabu la FIFA.

SOMA NA HII  GAMONDI AENDELEA KUWABURUZA SIMBA...AWAPIGA PIGO HILI JIPYA...KUBWA KULIKO