Home Azam FC DUBE HATIHATI KUIKOSA SIMBA KESHO AZAM COMPLEX

DUBE HATIHATI KUIKOSA SIMBA KESHO AZAM COMPLEX


VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kuna hatihati ya kupata huduma ya mchezaji wao Prince Dube ambaye ni kinara wa utupiaji.

Kesho Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi 64 itakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00 jioni.

Bahati amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo wa kesho na wanahitaji pointi tatu ila bado hawajajua kama wanaweza kumtumia Dube.

“Dube bado hajawa fiti kwa sasa hivyo lolote juu yake linaweza kutokea ila bado hakuna uhakika kuhusu uwepo wake kesho.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho na tunahitaji pointi tatu tupo tayari na kila mchezaji anajua kwamba tunahitaji pointi tatu kwa kuwa tunacheza na timu ambayo haina cha kupoteza.

“Licha ya kwamba wapinzani wetu mchezo wetu uliopita tulitoshana nguvu huu unakuwa mchezo mwingine,” .

Dube ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Azam FC akiwa ametupia mabao 14 na pasi za mabao ni mbili.

SOMA NA HII  AZAM FC YABAINISHA IKIKOSA UBINGWA BASI ITASEPA NA NAFASI YA PILI