Home Simba SC LWANGA AMZIDI UJANJA MKUDE NDANI YA SIMBA, KOCHA AFUNGUKA A-Z

LWANGA AMZIDI UJANJA MKUDE NDANI YA SIMBA, KOCHA AFUNGUKA A-Z


JONAS Mkude anatakiwa afanye kazi ya ziada mbele ya kiungo mkabaji, Thadeo Lwanga raia wa Uganda, anaonekana kukubalika na kocha wake Didier Gomes anayemuamini katika kikosi chake cha kwanza, tangu ajiunge na timu hiyo.

Wachezaji wa zamani wa timu hiyo, akiwemo kocha wa Kagera Sugar, Francis Baraza amewachambua Lwanga na Mkude utofauti wa majukumu yao na kumtaja nani anafiti zaidi nafasi hiyo.

Staa wa zamani wa timu hiyo ambaye sasa ni kocha, Emmanuel Gabriel alisema Lwanga ni mkabaji halisia alimfananisha na staa wa Manchester City, Fernandinho ambaye anacheza rafu nyingi kutoka na kazi yake ya kutoruhusu mpenyo wa kufikiwa mabeki wake.

“Lwanga nafananisha uchezaji wake na alivyokuwa James Kotei na alipoondoka Simba haikupata kiungo mkabaji halisi, akaja Fraga lakini naye akawa hakabi kivile ingawa alikuwa kiungo mkabaji halisi kama anavyokaba Lwanga kwasasa;

Kauli ya Gabriel ilipigiliwa msumari na beki wa zamani wa timu hiyo na Taifa Stars, Kasongo Athumani aliyesema kwamba, Lwanga anafanya kazi sahihi namba sita, anawasaidia mabeki wa kati Pascal Wawa na Joash Onyango kutokufanya makosa wala kupoteana.

“Mkude anachezea sana mipira, Lwanga ni mkabaji halisia anastahili nafasi hiyo.”

SOMA NA HII  SIMBA QUEENS WAZIDI KUTAKATA LIGI YA WANAWAKE...WAISASAMBUA FOUNTAIN GATE 4G....