Home Habari za michezo ISHU YA MCHEZAJI WA LIGI KUU KUTEKWA NA KUSHAMBULIWA NA VISU..UKWELI WOTE...

ISHU YA MCHEZAJI WA LIGI KUU KUTEKWA NA KUSHAMBULIWA NA VISU..UKWELI WOTE HUU HAPA…

Ligi Kuu Tanzania 2023/24

Watu wasiojulikana wamemteka na kumshambulia kwa kumpiga kwa vitu vyenye ncha kali mchezaji wa Geita Gold FC, Geofrey Rafael ‘Geofrey Muha’ na kumsababishia majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Geita, Sospeter Marwa amethibitisha kumpokea mchezaji huyo ambae amelazwa hospitalini hapo na kusema alipokelewa kwenye kitengo cha dharura saa tatu usiku wa Februari 19, 2024 akiwa na majeraha sehemu za usoni, mgongoni na mkono wa kulia.

Kwa mujibu wa Dk Marwa mchezaji huyo alikuwa kwenye mizunguko yake ya kawaida ndipo alipotekwa na watu hao na kumpeleka kusikojulikana na kumpiga na kumsababishia majeraha.

“Kweli yupo hapa tumempokea jana usiku saa tatu na nusu na tulimpa huduma ya kwanza ikiwa ni pamoja na kutibu majeraha na kumweka kwenye uangalizi na sasa anaendelea vizuri,” amesema Dk Marwa.

Katika taarifa kwa Umma iliyotolewa na klabu hiyo ikilaani tukio la kutekwa na kushambuliwa kwa mchezaji huyo, imeeleza mchezaji huyo alipatwa na madhila hayo kabla ya kuokolewa na wasamaria wema.

Alipotafutwa Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita, Adam Maro kuzungumzia tukio hilo amesema hawajapata taarifa za tukio hilo na kuomba apewe muda ili aweze kulifuatilia.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA AL AHLY...GAMONDI AWAPA MASTAA YANGA MAAGIZO YA 'KIGAIDI'...