Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA AL AHLY…GAMONDI AWAPA MASTAA YANGA MAAGIZO YA ‘KIGAIDI’…

KUELEKEA MECHI NA AL AHLY…GAMONDI AWAPA MASTAA YANGA MAAGIZO YA ‘KIGAIDI’…

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amewataka wachezaji wake kufa au kupona kupata pointi tatu kuelekea mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri ili kujiweka kwenye nafasi ya kusonga mbele .

Amesema walipoteza mechi ya kwanza kutokana na makosa yao na mechi yao ijayo ni muhimu kupambana ili kupata matokeo chanya kwa sababu wakipoteza nyumbani dhidi ya Al Ahly watakuwa na kazi kubwa.

Yanga imerejea nchini baada ya kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria na wako kambini kujiandaa na mchezo wa pili wa michuano hiyo dhidi ya wageni wao Al Ahly uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 1:00 usiku.

Kocha huyo ambaye amekuwa akifatilia mechi za wapinzani wao kila wanapocheza leo usiku atawafatilia Al Ahly ambayo inashuka dimba katika mchezo wa ligi ya Misri dhidi ya Smouha.

Gamondi alisema amekuwa akiwafatilia mechi za wapinzani wao wanapocheza ila kuona wapi anatakiwa kufanyia kazi na kuboresha kikosi chake kabla ya kukutana nao.

Alisema anafanya hivyo kila mechi pale mpinzani wake anapochezwa kabla ya kukutana nao, aliwaona Al Ahly wakicheza na Simba kwenye michuano ya Afrika Football League zote mbili Uwanja wa Mkapa na Misri.

“Nimewafatilia wapinzani wetu, wako vizuri tunatakiwa kuwa makini kwa sababu ya ubora wao, tulifanya makosa mechi iliyopita kwa kutokuwa na nidhamu ya mchezo na kupoteza.

Hii mechi kwetu ni muhimu kupata matokeo kwa sababu tutakuwa nyumbani na ikiwa kampeni yetu kushinda nyumbani ili kusonga mbele katika mashindano hayo,” alisema Kocha huyo.

Aliongeza kuwa kuna mambo matatu anayofanyia kazi ikiwemo umakini wa safu ya ulinzi na ushambuliaji pamoja na wachezaji kuwa na nidhamu ya mchezo wanapokuwa uwanjani.

Kocha huyo alisema kulingana na maandalizi ambayo wanaendelea kuyafanya kuelekea mchezo huo wanatarajia kufanya vizuri endapi vijana wake wakifuata maelekezo mazuri.

SOMA NA HII  MABOSI SIMBA WATANGULIA BOTSWANA,WAKWEPA HUJUMA, KAZI INAENDELEA