Home Habari za michezo HUU HAPA UKWELI KWANINI BOCCO HAACHIWI SIMBA…..KINACHOMLINDA HIKI HAPA…

HUU HAPA UKWELI KWANINI BOCCO HAACHIWI SIMBA…..KINACHOMLINDA HIKI HAPA…

Habari za Simba SC

Kwa nini John Bocco Simba? Si kazi ndogo kwa uongozi wa timu hiyo kumuacha straika huyo kirahisi, kutokana na heshima aliyojijengea tangu ajiunge na kikosi hicho 2017/18, akitokea Azam FC.

Bocco kacheza timu mbili tu za Ligi Kuu Bara (Simba, Yanga), jambo ambalo liliwahi kumfikirisha aliyekuwa meneja wa Azam, Philip Alando kwamba endapo Wanamsimbazi wakimuacha timu ipi itampa heshima yake.

“Maisha ya soka ni popote, lakini swali nililowahi kujiuliza ni Simba ikimuacha Bocco ni timu gani itamuaga kwa heshima, alipo sasa ama Azam, kutokana na maisha yake ya kutocheza timu nyingi.”

Hivi hapa vitu vitatu vinavyomfanya Bocco iwe ngumu kung’oka Simba, licha ya kuwepo kwa tetesi ndani ya misimu miwili za kutaka kuachana naye.

Msimu uliopita, Ihefu na Singida Fountain Gate zilikuwa zinasubiri tu aachwe ili ziweze kufaidi huduma yake, lakini ilishindikana akaendelea kusalia Msimbazi.

UONGOZI

Nje ya uwanja wachezaji wenzake wanamuelezea Bocco kuwa ana karama ya uongozi, ana uwezo wa kutatua mambo na wakati mwingine kuchukua hatua kwa watovu wa nidhamu, jambo linalompa nguvu kwa waajiri wake kuuona umuhimu wake kikosini.

Kati ya wachezaji waliowahi kukiri kuhusiana na Bocco kutatua matatizo yao ni aliyekuwa straika wa timu hiyo, Jean Baleke.

“Wakati najiunga na Simba nilikuwa sina pesa, Bocco alinipa pesa ndefu ya kujikimu, nilidhani ananikopesha kumbe kajitolea na alinipa moyo wa kupambana na kazi zangu,” alisema Baleke. Mchezaji mwingine ni straika wa kikosi hicho, Kibu Denis aliwahi kukiri kwenye moja ya mahojiano aliyofanya na chombo cha habari cha timu yake (Simba).

“Nakumbuka wakati napitia kwenye changamoto ya kutokufanya vizuri, Bocco alinikalisha chini na kuniambia, hakuna kitu kinaweza kudumu milele, nyakati zote zinapita, hivyo nisitoke mchezoni,” anasema.

Kipa wa Singida Fountain Gate, Beno Kakolanya wakati yupo Simba aliwahi kupata hekima za Bocco kama anavyoeleza: “Kuna kipindi aliniambia mimi ni kipa mzuri, niweze kuongeza elimu ya kusomea ukocha wa makipa utakaofanya niwe bora zaidi.”

Hizi hapa ni takwimu za Bocco.

MICHUANO YA CAF

Tangu ajiunge Simba 2017-2024 kacheza mechi za CAF 35, Ligi ya Mabingwa Afrika 26, mabao saba, asisti mbili, Kombe la Shirikisho Afrika, mechi saba, bao moja, asisti moja, African Football League mechi mbili, jumla ya dakika zote ni 1725.

WAMUONAVYO WENGINE

Straika wa zamani wa Yanga, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ mwenye rekodi ya kufunga mabao 143 ya Ligi Kuu anasema: “Bocco ni Mtanzania, lazima mchango wake aliouonyesha kwenye ligi uheshimiwe. Hakuna ambaye anaweza akadumu kwenye timu, ndio maana tulikuwepo tukaondoka. Ikifika wakati wake ataondoka watakuja wengine ambao watatakiwa kuandika rekodi zao.”

Nahodha wa Prisons Benjamin Asukile anasema: “Bocco anastahili heshima kubwa sana, naamini Simba hata ikiamua kuachana naye, itamuacha kwa heshima, kuna wakati nafikiria ni straika gani mbadala wake timu ya taifa.”

Beki wa Mtibwa Sugar, Oscar Masai anasema “Kati ya washambuliaji ambao nilikuwa nawahofia kwenye mechi akiwa kwenye kiwango cha juu ni Bocco, hujui anafunga saa ngapi, kwa mguu ama kichwa, anastahili heshima yake.”

SOMA NA HII  OKWI AWAPA MTU WA MAANA SIMBA...STEVE MUKWALA DEAL DONE