Home Habari za Simba Leo OKWI AWAPA MTU WA MAANA SIMBA…STEVE MUKWALA DEAL DONE

OKWI AWAPA MTU WA MAANA SIMBA…STEVE MUKWALA DEAL DONE

HABARI ZA SIMBA

STAA wa zamani wa Simba na Yanga, Emmanuel Okwi amehusika kwa kiasi kikubwa kumshawishi, Straika Mganda Steven Dese Mukwala (24) asaini Msimbazi.

Mukwala huenda akatambulishwa muda wowote kuanzia sasa kwani tayari yupo Jijini ametulia kwenye hoteli moja iliyoko kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Asante Kotoko ya Ghana, ambapo inaelezwa kila kitu kipo tayari na huenda akatambulishwa leo.

Mchezaji huyo msimu amefunga mabao 12 kwenye Ligi ya Ghana, na kwa mujibu wa Transfermarket dau lake la usajili linafika dola 175,000/= sawa na Tsh Milioni 456.

Timu alizowahi kuchezea hadi sasa ni, Vipers SC, Maroons FC, URA FC zote za Uganda, na Asante Kotoko.

Simba inaendelela kufanya mambo yake chini ya kapeti, huku ukitupia macho zaidi kwenye ukanda wa Afrika Magharib na nchini DR Congo, ili kujaribu kuona namna gani wanaweza kupata wachezaji wazuri.

Mpaka sasa mchezaji aliyesainiwa kutoka DR Congo ni Elie Mpanzu winga, anayetumia mguu wa kushoto na ana sifa ya  kupiga mashuti nje ya 18.

Muda wowote kuanzia sasa, anasubiri tu kukamilisha masuala ya mahitaji yakee,  ikiwemo sehemu ya kuishi hapa Tanzania.

Nguvu  ya Emmanuel Okwi kumvuta Simba mchezaji hiyo, ndiyo imefanikisha dili hilo kukamilika, na mwamba muda wowote atatambulishwa klabuni hapo.

SOMA NA HII  HAPA SIMBA WAVUNJE TU BENKI MAANA SIO KWA DAU HILI