Home Uncategorized MBELGIJI WA SIMBA APEWA TAHADHARI KIMATAIFA

MBELGIJI WA SIMBA APEWA TAHADHARI KIMATAIFA

 


ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amemtaka kocha mkuu wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck kwenda na tahadhari ya juu kuwakabili Platinum FC ya Zimbabwe kwa kuwa ni wazuri kuliko Plateau United ya Nigeria.

 

Simba imefanikiwa kutinga katika hatua ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwaondoa Plateau United ya Nigeria kwa jumla ya bao 1-0 na sasa wanatarajiwa kucheza ugenini na Platinum ya Zimbabwe Desemba 23, mwaka huu.

 

Rage amesema kuwa, Simba chini ya Sven raia wa Ubelgiji wanatakiwa kujiimarisha zaidi kadiri siku zinavyokweda kwa kuwa wapinzani wao Platinum ni wazuri ukilinganisha na Wanaigeria.


Simba inatakiwa ijipange vizuri katika hatua waliyofi kia kwani timu wanayokwenda kukutana nayo ni nzuri zaidi ya Wanaigeria waliopita hivyo hawatakiwi kuibeza hata kidogo, wanatakiwa wajipange kuhakikisha wanafanya vizuri.

 

“Kikubwa ninachokiona mimi waende wapambane wapate bao moja kisha walinde goli lao naona itakuwa na manufaa zaidi.


“Michuano hii jinsi ilivyo, kadiri unavyopiga hatua ndio mashindano yanavyokuwa magumu zaidi kwa kuwa unakutana na timu bora, hivyo wanahitaji kujipanga,” amesema Rage.

SOMA NA HII  MAKUNDI LIGI YA MABINGWA, SIMBA MIKONONI MWA WAARABU WA MISRI