Home Habari za Yanga Leo GUEDE, MUSONDA KUMPISHA SOWAH…INJINIA HERSI ASIMAMIA SHOW

GUEDE, MUSONDA KUMPISHA SOWAH…INJINIA HERSI ASIMAMIA SHOW

Habari za Yanga

YANGA ipo kwenye mazungumzo ya kumpata mshambuliaji raia wa Ghana, Jonathan Sowah kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Al-Nasr Benghazi ya Libya aliyojiunga nayo Januari mwaka huu kwa mkataba wa miaka miwili akitoka Medeama.

Inaelezwa endapo dili lake litakamilika, kuna uwezekano mkubwa wa Yanga kumuacha  Joseph Guede aliyejiunga Januari mwaka huu akitokea Tuzlaspor FC ya Uturuki na kufunga mabao sita ya Ligi Kuu Bara. Lakini hata Kennedy Musonda na yeye huenda akapigwa chini muda wowote wiki ijayo.

Taarifa za ndani zinasema chanzo cha maamuzi ya mabosi hao ni kutoridhishwa na namba zao za ufungaji katika michezo  waliyocheza msimu uliopita.

Yanga imewahi kukutana na Sowah msimu uliopita kwenye mechi mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama, mshambuliaji huyo akiwafunga Mabingwa hao kwa mikwaju wa penalti dakika ya 27, lakini Yanga walirudisha  kupitia kiungo wao Pacome Zouzoua, mechi hiyo ikiisha kwa bao 1-1.

Sowah aliwasumbua sana Yanga kwenye mechi hiyo, hatua ambayo ikawafanya mabosi wa timu kuendelea kufuatilia zaidi ingawa baadaye wakapunguza kasi baada ya kusajiliwa na timu nyingine dirisha dogo.

Yanga imepata taarifa kwamba Sowah ameachana na klabu yake ya Al-Nasr Benghazi ya Libya ambayo ameitumikia kwa miezi sita tu.

Sowah, ameandika barua ya kutaka kuachana na klabu yake na sasa akikamilisha mchakato huo tu atakuja nchini haraka kumalizana na Mabingwa hao mara tatu mfululizo Ligi Kuu Bara.

Sowah mwenyewe amefunguka kuwa, amefuatwa na Yanga na wako kwenye hatua ya mwisho kumalizana akisema tangu alipokutana na klabu hiyo imebaki moyoni kwake.

“Bado tunaongea na viongozi wa Yanga, tunaelekea mwisho kabisa kuna mambo namalizana na klabu yangu, yakifikia mwisho nitakuja hapo Tanzania haraka, unajua tangu nilipokutana nao mashabiki wa timu hiyo wamebaki kwenye moyo wangu,”alisema Sowah.

Tangu ajiunge na Al-Nasr Benghazi dirisha dogo Sowah ameifungia mabao matano ambapo mchezo ambao aling’aa ni ule dhidi ya Al Hilal Benghaz aliofunga mabao manne peke yake wakati timu yake ikishinda kwa mabao 6-3.

SOMA NA HII  YANGA KUMLETA CHID BENZ VS MADEAMA