Home Habari za Simba Leo KUELEKEA DABI YA KARIAKOO…MKUDE ATIBUA MAMBO.

KUELEKEA DABI YA KARIAKOO…MKUDE ATIBUA MAMBO.

Habari za Yanga leo

KIUNGO wa Mpira Jonas Mkude anayekipiga ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa hana hofu na Kariakoo Dabi kutokana na uzoefu alionao muda wowote yupo tayari kuchezwa kwani hiyo ni kazi yake.

Ikumbukwe kwamba Mkude ni timu mbili kubwa amecheza kwa sasa katika ardhi ya Tanzania, alianza na Simba kisha akaibukia Yanga baada ya kukutana baada ya kutemwa na Simba.

Oktoba 19 2024 mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Simba na Yanga unatarajiwa kuchezwa ikiwa ni mzunguko wa kwanza kwa wababe hao kukutana uwanjani kwenye mchezo wa Ligi kuu ya NBC.

Mkude amesema kila wakati wanafanya maandalizi kwa ajili ya mechi zao zote ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Simba kwa kuwa upo kwenye ligi.

“Kuhusu Kariakoo Dabi naona ni mchezo wenye ushindani mkubwa lakini sina hofu kucheza yaani muda wowote nipo tayari kwa kuwa ni maisha yangu kucheza mpira sina hofu na ninatambua kwamba mpira ni kazi ambayo ninaifanya kwa namna yoyote mashaka hapana.

“Mazoezi na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ni kitu muhimu na tunashirikiana wachezaji wote, benchi la ufundi linatambua nani anapaswa kuanza na kipi kinapaswa kufanyika kuelekea kwenye mchezo huo.”

Yanga imecheza mechi nne za ligi ambazo ni dakika 360 ikikomba pointi tatu kila mchezo na kufikisha jumla ya pointi 12 kibindoni ni mabingwa watetezi wa ligi.

SOMA NA HII  WYDAD WAJIPANGA KUISHAMBULIA SIMBA KWA KASI...KOCHA ACHEZE NA PLAN B