Home Uncategorized KISA YANGA, SIMBA YAMKOMALIA CHAMA, YATAJA MUDA WA MKATABA WAKE

KISA YANGA, SIMBA YAMKOMALIA CHAMA, YATAJA MUDA WA MKATABA WAKE


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kiungo wao Clatous Chama raia wa Zambia mkataba wake bado unaishi mpaka pale Juni 2021.

Chama amekuwa akihusishwa kujiunga na wapinzani wa Simba Yanga ambao inaelezwa kuwa wameanza kufanya mazungumzo na nyota huyo ambaye kwa sasa yupo nchiniZambia.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amekanusha taarifa kuhusu mkataba wa kiungo  Chama kumalizika mwaka huu, akisisitiza kuwa mkataba wa nyota huyo utamalizika mwezi Juni mwaka 2021.

“Timu yoyote itakayoanza kufanya mazungumzo na Chama itakuwa ni kinyume na utaratibu wa Shirikisho la Soka duniani (Fifa) hivyo walioanza waache mara moja.

“Tunajua kwamba ni mchezaji mzuri lakini bado ni mali ya Simba kwa sasa labda kama walikuwa hawajui bado ni mali yetu na haendi popote pale,” amesema.

SOMA NA HII  FERGUSON AMPA BONGE LA MTIHANI MENEJA WA ARSENAL