Home Uncategorized BANDA:TUNAPIGA MATIZI KAMA KAWAIDA HUKU

BANDA:TUNAPIGA MATIZI KAMA KAWAIDA HUKU


ABDI Banda, beki wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars anayekipiga Highlands Park FC ya Afrika Kusini amesema kuwa bado wanapiga matizi kama kawaida na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.

 Ligi Kuu ya Afrika Kusini imesimamishwa kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia kwa sasa.

Banda amesema kuwa:-“Tupo tunachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona na tunafanya mazoezi ili kulinda vipaji vyetu kwa makundi ila ni kwa njia ya mtandao.

“Benchi la ufundi limegawa wachezaji kwa makundi ya wachezaji watanowatano mpaka sita ambapo kila mchezaji anaona namna anavyotakiwa kufanya mazoezi yake binafsi akiwa nyumbani,”.

SOMA NA HII  MBWANA SAMATTA AMPIGA MKWARA KIBA KUELEKEA NIFUATE