Home Simba SC SIMBA KUYAKOSA MABAO 42 NDANI YA LIGI KUU BARA MAZIMA

SIMBA KUYAKOSA MABAO 42 NDANI YA LIGI KUU BARA MAZIMA


 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba msimu ujao watayakosa mabao yao 42 ndani ya ligi baada ya nyota ambao walihusika katika mabao hayo kupigwa bei mazima.

Ni Luis Miqissone alifunga mabao 9 na pasi 10 huyu tayari ameshaaga ndani ya kikosi hicho na msimu ujao wa 2021/22 hatakuwa ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu Didier Gomes.


Atakumbukwa na mashabiki wa Simba na Tanzania kwa ujumla kwa namna ambavyo aliweza kuwa mpambanaji wa muda wote ndani ya Simba. Kwenye mchezo wa machozi na damu mbele ya Tanzania Prisons alifunga bao dakika za lala salama na kuwafanya Simba wagawane pointi mojamoja na Prisons Uwanja wa Mkapa.



Pia kadi yake ya njano ambayo alionyeshwa msimu huu ilikuwa ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania ambapo alifunga bao lake la kwanza kwa msimu kati ya 9 alikuwa nje ya 18 na kitendo chake cha kushangilia kwa kuwafuata mashabiki mwamuzi alitafsri kwamba ni utovu wa nidhamu akamuonyesha kadi ya njano.

Ni yeye aliyetimiza majukumu yake kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Yanga wakati wakisawazisha dakika za lala salama bao lililofungwa na Michael Sarpong na alitoa pasi hiyo Luis kwa pigo la kona akiwa nje ya 18 ikakutana na kichwa cha Joash Onyango.

Kwa upande wa Chama, huyu ni mfalme wa pasi za mwisho akiwa na tuzo ya mchezaji bora wa ligi wa msimu wa 2019/20 ambapo msimu huo alifunga mabao mawili na pasi 10 za mabao jambo lililofanya awepo pia kwenye orodha ya kikosi bora cha msimu pia alisepa na tuzo ya kiungo bora.

Msimu wake wa 2020/21 ambao ulikuwa ni wa mwisho kwake alifunga mabao 8 na kutoa pasi 15 akiwa ni namba moja kwa watengeneza pasi za mwisho naye pia hatakuwepo ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao.

Kwa ujumla nyota hawa katika mabao 78 ya Ligi Kuu Bara yaliyofungwa msimu uliopiita walihusika kwenye mabao 42. Luis anatajwa kuibukia ndani ya Al Ahly ya Misri na Chama anatajwa kuibukia RS Berkane ya Morocco.

Maisha yanakwenda kasi na Simba wenyewe wamethibitisha kwamba miamba hiyo haitakuwepo msimu ujao wa 2021/22.
SOMA NA HII  PAMOJA NA USHINDI WA JANA....SIMBA WALIA NA HILI 'KUBWA'....TAARIFA YATUMWA TFF...