Home Habari za michezo PAMOJA NA USHINDI WA JANA….SIMBA WALIA NA HILI ‘KUBWA’….TAARIFA YATUMWA TFF…

PAMOJA NA USHINDI WA JANA….SIMBA WALIA NA HILI ‘KUBWA’….TAARIFA YATUMWA TFF…

Habari za Simba leo

LICHA ya kuvuna pointi tatu muhimu dhidi ya JKT Tanzania , Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa mazingira ya uwanja imesababisha kutocheza kandanda safi ambayo ilizoeleka ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Simba walikuwa ugenini dhidi ya wenyeji wao JKT Tanzania katika mchezo wa 15 wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuibuka na ushindi wa 1-0, uwanja wa Maj General Isamahyo, Mbweni, bao pekee lilifungwa na Clatous Chama.

Kocha wa makipa wa Simba, Daniel Cadena amesema kulingana na mazingira ya uwanja waliocheza kupeleka wachezaji kutocheza kwa ubora ulizoeleka kwa mashabiki na kushindwa kumiliki mpira hasa kipindi cha pili.

Amesema anafurahi kuona wachezaji wamepambana na kuyafanya yale waliyowaelekeza katika uwanja wa mazoezi na kuhamisha kwenye mechi na kufanikiwa kuvuna pointi tatu muhimu.

“Kikubwa ni pointi tatu bila kuangalia ni ushindi wa aina gani, tumecheza vizuri na tumefanya mzunguko wa baadhi ya wachezaji akiwemo kuanza na Kibu (Dennis) namba 9 licha ya wanaocheza nafasi hiyo walikuwa benchi hii ni baada ya kuwepo kwa mfululizo wa mechi.

Tuliwapa nafasi ya wachezaji kupumzika na kuwapa nafasi ya kuingia katika kipindi cha pili na kufanikiwa kuvuna pointi tatu muhimu na kuendelea katika vita vya mbio za kuwania ubingwa wa ligi hiyo,” amesema Cadena.

Ameongeza kuwa kila mechi inekuwa na mzunguko wa wachezaji kila mechi kuwepo mabadiliko machache kwa sababu ya kila mchezaji kupata nafasi ya kucheza na kusaidia timu kupata matokeo mazuri na kufikia malengo yao.

Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Hamsini Malale amesema mechi imekamilika na wamekubali matokeo waliyoyapata kwa kukubali kupoteza mbele ya Simba kulingana ubora wa safu ya viungo.

“Simba walitizidi katika kiungo na kipindi cha pili tulibadilika na kuwafanya Simba kuzuia sana pale tunapokuwa na mpira, tulitengeneza nafasi tatu hatukuzitumia lakini Simba walipata mbili moja ikazaa bao.

Hii ni kwa sababu washambuliaji wangu hawakuwa makini na utulivu wanapokuwa katika lango la mpinzani tunarudi uwanja wa mazoezi kusahihisha makosa yetu na kujiandaa kwa mechi ijayo,” amesema Malale.

SOMA NA HII  WAKATI LA CHAMA LIKIWA LA MOTO....NTIBAZONKIZA NAYE AWAVIMBIA MABOSI SIMBA...ISHU HII HAPA...