Home Azam FC AZAM FC SERA YAO MPYA NI MWENDO WA KIMYAKIMYA

AZAM FC SERA YAO MPYA NI MWENDO WA KIMYAKIMYA


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa msimu huu watakua na mwendo wa toauti tofauti na msimu mpya hivyo sera yao ambayo wameizindua itawafanya wafanye mambo mengi makubwa.

Agosti 16, Azam FC ilitambulisha sera yao rasmi ambayo itatumika kwa msimu wa 2021/22 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Msimu uliopita wa 2020/21 Azam FC ilikuwa na sera inayokwenda kwa Azam FC tuna jambo letu na iliwafanya waweze kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Walikusanya kibindoni pointi 68 na kufunga mabao 50 huku wao wakiokota nyavuni mabao 22.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit, ‘Zakazakazi ‘ amesema kuwa msimu huu wanakuja na sera mpya watakayotumia tofauti na ile ya msimu uliopita.

“Tulikuwa na ‘Jambo letu’ msimu uliopita ila kwa msimu ujao tutakuwa na slogan ya ‘Kimyakimya’ katika mambo ambayo tunayafanya.

“Ndio maana unaona kwamba tumekuwa na mambo kimyakimya, tumezundua nembo mpya na hatujawa na kelele nyingi kwa sasa na bado tunaendelea,”

Pia Azam FC imetambulisha nafasi mpya kwenye sekta ya mpira ndani ya Tanzania ambayo ni ile ya Mkurugenzi wa Mpira iliyopo mikononi mwa Dr. Jonas Tiboroha aliyepewa dili la mwaka mmoja.
SOMA NA HII  AZAM KUANZA MAZOEZI KESHO