Home Habari za michezo PAMOJA NA KUFUNGA ‘HAT-TRICK’ JUZI…MAYELE AKOLEZA MSIMAMO WAKE DHIDI YA YANGA KWENYE...

PAMOJA NA KUFUNGA ‘HAT-TRICK’ JUZI…MAYELE AKOLEZA MSIMAMO WAKE DHIDI YA YANGA KWENYE MECHI ZA CAF…


STRAIKA wa Yanga, Fiston Mayele ameanza kufukuzia moto wa kuvunja ufalme wa lejendi, Mrisho Ngassa ambaye ndiye aliweka rekodi ya kufunga hat-trick kwa timu za Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ngassa alianza kufunga hat-trick ya kwanza Februari 8, 2014 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine ya Comoro, Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 7-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa, hakuishia hapo akafunga nyingine kwenye  mchezo wa marudiano Wanajangwani wakishinda mabao 5-2 ugenini.

Ngassa ambaye alikuwa kwenye kiwango cha juu wakati huo, mchezo mwingine wa CAF alifunga hat trick ya mabao  manne, Yanga ikishinda mabao 6-0 dhidi ya Etoile d’or ilikuwa Februari 15, 2016. Imepita miaka sita tangu Ngasa afunge hat -trick ya mwisho 2016, ambapo Mayele amefunga ya kwanza dhidi ya Zalan ya Sudan Kusini.

Mayele amefunga hat -trick hiyo, Yanga ikishinda mabao 4-0 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa huku akiweka mpira kwenye tumbo lake na kunyonya kidole kuashiria anatarajia kupata mtoto.

SOMA NA HII  KWA BENCHIKHA HUYU.....WANASIMBA TARAJIENI MAMBO HAYA MATANO MAKUBWA....