Home Habari za michezo CAF WAPANGA ‘MAPROO’ BONGO KUKIPIGA DHIDI YA TAIFA STARS…MCHONGO MZIMA UKO HIVI…

CAF WAPANGA ‘MAPROO’ BONGO KUKIPIGA DHIDI YA TAIFA STARS…MCHONGO MZIMA UKO HIVI…

Taifa Stars

Kama watakuwemo kwenye vikosi vya timu zao za taifa vitakavyoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani huko Ivory Coast, Fiston Mayele na Clatous Chama watacheza dhidi ya marafiki zao watakaokuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Hiyo ni kufuatia timu zao za taifa, Zambia na DR Congo kupangwa kwenye kundi moja na Taifa Stars katika fainali hizo zitakazoanza Januari 13 hadi Februari 11 huko Ivory Coast.

Katika droo iliyochezeshwa jana saa 4 usiku huko Abidjan, Ivory Coast, timu hizo tatu zimepangwa katika kundi F sambamba na Morocco.

Timu hizo zote tatu zilizopangwa na Taifa Stars katika kundi F, zina historia kubwa ya kutamba katika fainali hizo ambapo zote zimewahi kutwaa taji la Afcon kwa nyakati tofauti.

Morocco ‘Simba wa Atlas’ ni mabingwa wa Afcon mwaka 1976 na mwaka uliopita walitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia huko Qatar.

Zambia ‘Chipolopolo’ imewahi kutwaa taji la Afcon mara moja ambayo ni mwaka 2012 lakini wamewahi kumaliza katika nafasi ya pili mwaka 1974 na 1994.

DR Congo nao wamekuwa sio wanyonge katika Afcon kwani wamewahi kutwaa taji mara mbili ambazo ni 1968 na 1974.

Kundi A la mashindano hayo mwakani litakuwa na wenyeji Ivory Coast, Nigeria, Guinea ya Ikweta na Guinea Bissau wakati kundi B lina timu za Misri, Ghana, Cape Verde na Msumbiji.

Mabingwa watetezi Senegal wao wamepangwa kundi C pamoja na Cameroon, Guinea na Gambia na kundi litakuwa na Algeria, Burkina Faso, Mauritania na Angola.

Majirani wawili wa Kusini mwa Afrika, Afrika Kusini na Namibia wamepangwa katika kundi E pamoja na tai wa Kaskazini mwa Afrika, Tunisia na Mali ya kipa wa Yanga, Djigui Diarra

Kundi A: Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea, Guinea-Bissau
Kundi B: Misri, Ghana, Cape Verde, Msumbiji
Kundi C: Senegal, Cameroon, Guinea, The Gambia
Kundi D: Algeria, Burkina Faso, Mauritania, Angola
Kundi E: Tunisia, Mali, Afrika Kusini, Namibia
Kundi F: Morocco, DR Congo, Zambia, Tanzania

Bingwa mtetezi katika michuano hiyo ni Senegal, wakati Misri itaingia uwanjani ikiwa ndio timu inaongoza kwa kulibeba mara nyingi taji hilo yaani mara 7, ikifuatiwa na Cameroon (5) kisha Ghana (4)

SOMA NA HII  ISHU YA MBRAZILI KUSEPA KAMBI YA SIMBA UTURUKI...UKWELI USIOSEMWA HUU HAPA...