Home Ligi Kuu VITA YA KUSHUKA DARAJA, RATIBA KAMILI HII HAPA

VITA YA KUSHUKA DARAJA, RATIBA KAMILI HII HAPA


JULAI 18 leo inatarajiwa kuwa vita kwa timu ambazo zinapambania nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa tayari bingwa ameshapatikana ambaye ni Simba.

Matokeo ya leo yataamua nani atakuwa nani kwa kuwa ni mechi za mwisho na lazima timu nne zitashuka jumlajumla na kushiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.

Hii hapa ratiba kamili na namna vita yao itakavyokuwa:-

 Coastal Union v Kagera Sugar

Coastal Union ikiwa imetoka kushinda mabao 5-0 mbele ya Mwadui ambayo imeshuka daraja inawakaribisha Kagera Sugar ambao wametoka kushinda bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania,utachezwa  Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Coastal Union bado haina uhakika wa kubaki kwenye ligi kwa kuwa ina pointi 37 ikiwa nafasi ya 14 inakutana na Kagera Sugar lliyo nafasi ya 11 na pointi 40 ambayo nayo inahitaji pointi tatu kujihakikishia nafasi ya kubaki ndani ya ligi.

Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union ameliambia Championi Jumamosi kuwa bado wanaendelea kupambana mpaka mwisho wa ligi.

Kwa upande wa Francis Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar aliliambia Championi Jumamosi kuwa anahitaji kuibakisha timu hiyo kwenye ligi msimu ujao.

Dodoma Jiji v Yanga

Dodoma Jiji ikiwa imetoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 7 na pointi zake ni 43 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya pili na imetoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

JKT Tanzania v Mtibwa Sugar

JKT Tanzania ikiwa imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 5-2 dhidi ya KMC ipo nafasi ya 15 na pointi 36 inapambana kupata pointi tatu ili kuona hatma yao itakuwaje kama wanaweza kucheza mechi za mtoano inakutana na Mtibwa Sugar yenye pointi 39 ipo nafasi ya 13 utachezwa Uwanja wa Samora, Iringa.

Mohamed Abdalah, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania alisema kuwa watayafanyia kazi makosa yao kwa kupoteza mbele ya KMC ili kupata pointi tatu na Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kuwa wanahitaji pointi tatu za JKT Tanzania.

KMC V Ihefu

KMC ikiwa ipo nafasi ya tano na pointi 45 baada ya kucheza jumla ya mechi 33 inakutana na Ihefu iliyo nafasi ya 16 na pointi 35 haina uhakika wa kubaki ndani ya ligi hivyo itapambana kupata pointi tatu huku ikisikilizia matokeo ya JKT Tanzania  na Coastal Union itakuwa ni Uwanja wa Uhuru.

SOMA NA HII  MAPILATO WA SIMBA V YANGA, WACHEZAJI WAJIANDAE KISAIKOLOJIA

Habib Kondo, Kocha Msaidizi wa KMC aliliambia Championi Jumamosi kuwa wachezaji wanajua kwamba kinachohitajika ni ushindi na Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila alisema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanahitaji pointi tatu.


Mbeya City v Biashara United

Mbeya City ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Gwambina FC ina pointi 39 kibindoni ikiwa nafasi ya 12 inakutana na Biashara United iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Prisons ipo nafasi ya nne na pointi zake ni 50 itakuwa ni Uwanja wa Sokoine.

Nyota wa Mbeya City, Kibu Denis aliliambia Championi Jumamosi kuwa maandalizi yapo vizuri kwa ajili ya mchezo huo na Ofisa Habari wa Biashara United, Idrisa Sechombo alisema kuwa wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo.

Ruvu Shooting v Azam FC

Ruvu Shooting ikiwa imetoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya Namungo FC kibindoni ina pointi 41 ipo nafasi ya 10 inakwenda kukutana na  Azam FC ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Simba.

Mchezo wao uliopita Uwanja wa Azam Complex walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2. Azam FC ipo nafasi ya tatu ina pointi 65 itakuwa ugenini Uwanja wa Mabatini.

Masau Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting alisema kuwa hakuna namna ambayo Azam FC wanaweza kukwepa kufungwa huku Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati akiweka wazi kwamba wanajua mchezo utakuwa mgumu ila malengo yao ni kushinda.

Simba v Namungo, Uwanja wa Mkapa

Mabingwa wa ligi watakabidhiwa taji lao leo, Uwanja wa Mkapa kwa kusaka ushindi mbele ya Namungo FC ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Ruvu Shooting.

Dider Gomes, Kocha Mkuu wa Simba aliliambia Championi Jumamosi kuwa hakuna namna ambayo wanapaswa kufanya kwenye mchezo wao wa mwisho zaidi ya kupata ushindi.

Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia alisema kuwa wachezaji wana morali kubwa na wanaamini kwamba watashinda mchezo huo.

Tanzania Prisons v Gwambina  

Tanzania Prisons ikiwa nafasi ya 6 na pointi 43 inakutana na Gwambina FC  yenye pointi 34 ipo nafasi ya 17.