Home Yanga SC FEI TOTO: SIMBA WEPESI TU, ATUMA UJUMBE MZITO

FEI TOTO: SIMBA WEPESI TU, ATUMA UJUMBE MZITO


KIUNGO mchezeshaji kipenzi cha Yanga, Salum Abdallah ‘Fei Toto’, hana hofu na mchezo wa 
fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), maarufu kama FA watakaocheza dhidi ya Simba kwani hizo ndiyo mechi zake anazotamani kuzicheza.

Kauli hiyo huenda ikawa salamu kwa viungo wa Simba atakaokutana nao tena katika mchezo huo ambao ni Luis Miquissone, Clatous Chama,Larry Bwalya na Taddeo Lwanga atakaokutana nao.

Timu hizo zinatarajiwa kukutana kwa mara ya pili katika mchezo huo wa fainali utakaopigwa Julai 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika wa mkoani Kigoma.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Fei Toto alisema kuwa kwake michezo yote dhidi ya Simba ni miepesi kwake na anaichukulia kawaida tofauti na akikutana na timu ndogo.

Fei Toto alisema katika michezo yote iliyopita dhidi ya Simba alicheza chini ya presha kutokana na kufahamu uwezo wa kila mchezaji.

Aliongeza kuwa michezo dhidi ya timu ndogo inampa ugumu kutokana na kutowajua wachezaji wa timu pinzani. Hivyo ni katika kuelekea fainali ya FA, hana hofu ya mchezo na wataingia uwanjani kwa ajili ya kupata matokeo mazuri ya ushindi pekee.

“Mechi hizi za Kariakoo Dabi, mashabiki ndiyo wanaifanya kuwa ngumu kutokana na presha kubwa wanazokuwa nazo kabla ya mchezo husika.

“Kama wachezaji nikiwemo mimi mwenyewe sijawahi kuona ugumu wowote wa Kariakoo Dabi, ninacheza bila ya presha yoyote huku nikitimiza majukumu yangu ya uwanjani kuchezesha timu, kutengeneza mabao na kuzuia mashambulizi.

“Binafsi hizi ndogo ndiyo zinanipaga ugumu kila tunapokutana nazo uwanjani, kwani wachezaji wao wengi hatuwafahamu, hivyo wanatupa ugumu katika kupata matokeo,” alisema Fei Toto.

SOMA NA HII  MAYELE : SUDAN PALIKUWA PAGUMU SANA...LAZIMA TUFANYE JAMBO...