Home CAF AL AHLY YASEPA NA TAJI LA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

AL AHLY YASEPA NA TAJI LA LIGI YA MABINGWA AFRIKA


 KLABU ya Al Ahly ya Misri imefanikiwa kutetea taji lake la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ubao wa Uwanja wa Mohammed V kusoma Kaizer Chief 0-3 Al Ahly kwenye mchezo wa fainali uliochezwa usiku wa kuamkia leo.

Kipindi cha kwanza ngoma ilikuwa nzito kwa timu hizo zote ambazo ziliwahi kucheza na Klabu ya Simba ya Tanzania kwa nyakati tofauti ambapo Al Ahly mabingwa walicheza na Simba katika hatua ya makundi na Kaizer Chiefs ilicheza na Simba katika hatua ya robo fainali.

Ni mabao ya Mohamed Sherif dk 53, Mohamed Magdy Afsha dk 64 na Amr El Solia dk 74 yalitosha kuwapa taji hilo waarabu hao wa Misri.

Nyota wa Kaizer Chiefs, Happy Mashiane hakuweza kumaliza fainali hiyo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu dk 45+4 na kuwafanya wacheze wakiwa pungufu washkaji zake.

Jumla mashuti ambayo Al Ahly ilipiga yalikuwa ni 17 na mashuti manne yalilenga lango huku Kaizer Chiefs ikipiga mashuti matatu na ni moja ambalo lililenga lango.


SOMA NA HII  MAGOLI BORA CAF: FRIII KIKI YA CHAMA YAPIGIWA SALUTI CAF...ULE MSHUTI WA KANOUTE SASA