Home Habari za michezo MAYELE : SUDAN PALIKUWA PAGUMU SANA…LAZIMA TUFANYE JAMBO…

MAYELE : SUDAN PALIKUWA PAGUMU SANA…LAZIMA TUFANYE JAMBO…

Habari za Yanga

Straika wa Yanga, Fiston Mayele amesema mazingira magumu waliyokutana nayo kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Al Hilal ya Sudan ndiyo yaliyochangia wao kupoteza mchezo huku viongozi wakisisitiza kuweka nguvu michezo yao ijayo ikiwemo mechi yao na watani, Simba itakayochezwa Oktoba 23, mwaka huu.

Yanga iliondolewa kwenye mashindano hayo kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 Dare es Salaam na kulala 1-0 katika marudiano.

Akizungumza mara baada ya kutua nchini wakitokea Sudan, Mayele alisema ugenini walikutana na mazingira magumu ambapo wapinzani wao walitumia vizuri uwanja wa nyumbani na kupata bao la mapema ikiwa ni tofauti na mechi iliyochezwa Kwa Mkapa.

“Wachezaji tumekutana na kufanya kikao kizito ikiwemo sisi wenyewe kuhimizana zaidi kila mmoja kufanya vizuri katika michezo iliyo mbele yetu na kusahau yaliyotokea huko Sudan,” alisema Mayele na kuongeza;

“Wachezaji kila mmoja ameonyesha kuumizwa na matokeo haya ila tunakusanya nguvu kwa pamoja kurudi na matokeo bora kwenye Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na mashindano ya ndani.”

SOMA NA HII  KAMA UNAUNDUGU NA MCHEZAJI WA YANGA...'CHAP HARAKA KAOMBE MSAADA'...WAMELIPWA PESA ZAO KIMYA KIMYA AISEE...