Home Habari za michezo HUU HAPA UJUMBE BACCA KWA ATEBA BAADA YA KUSHINDWA KUIFUNGA YANGA JUZI…

HUU HAPA UJUMBE BACCA KWA ATEBA BAADA YA KUSHINDWA KUIFUNGA YANGA JUZI…

Habari za Yanga leo

BEKI wa Yanga, Ibrahim Bacca amemtumia ujumbe mshambiliaji wa Simba, Leonel Ateba akimtaka aweke akiba ya maneno na afahamu kwamba soka ni vitendo zaidi na sio maneno.

Kauli hiyo ya Bacca ni baada ya kufanikiwa kumzuia Ateba kutofunga bao katika mchezo wa Jumamosi, Oktoba 19 uliomalizika kwa Yanga kuifunga Simba bao 1-0. Kauli ya Bacca ni baaada ya hivi karibuni Ateba kuwachimba mkwara mabeki wa Yanga akiwaambia kuwa lazima awafunge bila kutaka kujua majina yao.

Bacca amesema tambo za Ateba zilimuamsha usingizini na kuongeza umakini zaidi katika mchezo huo na ndio maana kwa kushirikiana na wachezaji wenzake walifanikiwa kumfunga mdomo.

Ameongeza kuwa mchezaji anapaswa kumuheshimu mpinzani wake kwani katika soka hakuna maneno bali ni vitendo zaidi.

“Ninavyohisi alikuwa anajipa motisha, alikuwa anajifariji ili ahakikishe mechi hii anafanya vizuri, lakini nimwambie yupo vizuri ila aweke akiba ya maneno,” amesema Bacca.

SOMA NA HII  KIWANGO CHA CHAMA CHAZUA GUMZO MORO...PABLO APAGAWA..AMPA RASMI MAJUKUMU MAPYA...