Home Habari za michezo HIZI HAPA KAULI 3 TATA ZA MAGORI BAADA YA SIMBA ‘KUBANJULIWA’ 1-0...

HIZI HAPA KAULI 3 TATA ZA MAGORI BAADA YA SIMBA ‘KUBANJULIWA’ 1-0 NA YANGA JUZI…

Habari za Simba

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba Crescentius Magori bado ameendelea kuwa gumzo mitandaoni baada ya kuendelea kutoa kauli tata juu ya matokeo ya kikosi cha Simba kwenye mchezo dhidi ya Yanga Oktoba 19 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Baada ya mchezo huo, kupitia ukurasa wake wa Instagram Magori alichapisha ujumbe wa kumlaumu golikipa wa Simba akiamini kwamba amefanya uzembe wa kiwango cha juu mno.

“Musa Camara, Musa Camara nakuita mara 3!! Tutajua very soon! Hata huko Conakry tutafika! “

Hakuishia hapo alimshushia lawama mwamuzi wa mchezo huo Ramadhan Kayoko akiamini kuwa hakuitendea haki timu yake.

“Kayoko Kibu kaangushwa mara 2 ndani ya 18 hukutoa penati unaenda kutoa faulo haina kichwa wala miguu!!” aliandika Magori.

Magori alirejea tena na chapisho jingine akiwalaumu wenye haki ya matangazo ya Televisheni akisema kuwa wamefumbia macho makosa ya mwamuzi kwani anaamini walikuwa na sauti ya kuyasemea makosa hayo.

Siku ya jana ikaisha kwa machapisho hayo mawili lakini mapema Oktoba 20, Magori amechapisha ujumbe mwingine akisema kuwa aliyoyafanya jana alikusudia na wala sio hasira za kupoteza mchezo hivyo leo ataweka mambo yote hadharani.

“Mlifikiri ni hasira za jana hapana, leo nitaongea” ameandika Magori.

Bado wadau wa soka wanasubiri atakachokizungumza Magori kwani amesisitiza ni lazima leo avunje ukimya.

SOMA NA HII  KUMBE! WACHEZAJI WAMEMGOMEA MKUDE SIMBA