Home Habari za Simba Leo SIMBA YATANGAZA VITA BAADA YA KUICHAPA PRISONS…FADLU AHUSIKA NA MCHONGO

SIMBA YATANGAZA VITA BAADA YA KUICHAPA PRISONS…FADLU AHUSIKA NA MCHONGO

KLABU ya Simba SC wakiwa uwanja wa Sokoine Mbeya wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Bao pekee la Simba SC na la ushindi lilifungwa na beki Mcameroon, Che Fondoh Malone Junior dakika ya tano tu ya mchezo akimalizia mpira uliomponyoka kipa kipa Adam Mbise kufuatia shuti la mpira wa adhabu la kiungo Kibu Denis Prosper.

Kwa ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 16 katika mchezo wa saba na kusogea nafasi ya tatu, nyuma Singida Black Stars yenye pointi 19 baada ya wote kucheza mechi saba, huku Yanga akiwa na nafasi ya pili na alama 18 akiwa amecheza michezo 6.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUWA IHEFU....'JINAMIZI' LA SIMBA LAZIDI KUMSUMBUA OKWA...AFUNGUKA A-Z...