Home Habari za michezo KUMEKUCHA SIMBA…ACHANA NA MANZOKI…STRAIKA HILI LA MABAO LANUKIA MSIMBAZI…

KUMEKUCHA SIMBA…ACHANA NA MANZOKI…STRAIKA HILI LA MABAO LANUKIA MSIMBAZI…

Mabosi wa Simba chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ na benchi la ufundi wamekubaliana kufanya usajili wa kwanza mapema na haraka iwezekanavyo kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Desemba 15.

Simba tangu ameondoka straika asilia, Dejan Dejan Georgijevic baada ya kuvunja mkataba kwenye nafasi ya mastraika imebaki na John Bocco na Habibu Kyombo ambao si wachezaji wa kikosi cha kwanza huku Phiri anayecheza mara kwa mara hapo si nafasi yake asili.

Katika kuhakikisha Simba inapata straika mzuri mwenye uwezo wa kufunga taarifa zinadai kuwa mabosi wa timu hiyo chaguo lao la kwanza mshambuliaji wa Dalian Professional ya China, Cesar Lobi Manzoki.

Manzoki alisainiwa na Simba mkataba wa miaka miwili(kwa siri sana) kutokea Vipers ya Uganda ila ilikuwa ngumu kumpata kutokana na timu hiyo kuhitaji mkwanja mrefu zaidi kwa sababu iliyoeleza bado anamkataba.

Inadawaiwa ilitumika akili kumpeleka China na alisaini mkataba wa miezi minne huko ili atue Simba dirisha dogo la usajili ila suala hilo linaweza kuwa gumu na kuingia doa kwani Manzoki analipwa pesa nyingi mara nne ya ile atakayokuja kulipwa Msimbazi.

Kwenye kulitambua hilo mabosi wa Simba pamoja na Mgunda imeanza kuwafuatilia mastraika mbalimbali ikiwemo, Mghana Kwame Opoku mchezaji wa USM Alger ya Algeria aliyetolewa kwa mkopo Najran ya Saudi Arabia.

Kama Mgunda pamoja na mabosi wa Simba wataridhika na kiwango cha Opoku haswa kwenye kufunga mabao anaweza kuchukuliwa kwani atacheza hadi mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambako Simba inasubiri makundi yapangwe Jumatano.

Mgunda alisema amewaeleza mabosi zake haraka iwezekanavyo wanatakiwa kusajili mshambuliaji asilia mwenye uwezo wa kufunga kutokana timu yake imekuwa na shida kwenye eneo hilo.

Alisema; “ Kama umeangalia tangu nimechukua Simba imekuwa na shida kwenye kufunga mabao ingawa kwenye mchezo mmoja zinatengenezwa nafasi si chini ya tano zinapotea au kutumiwa chache tofauti zinavyopatikana.”

“Nahitaji mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga kwani timu yangu inatengeneza nafasi nyingi za kufunga zinapotea, nikimpata huyo na straika mapema kabla ya dirisha dogo la usajili naimani tutakuwa na mabadiliko ndani ya timu yetu,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Tayari kuna mastraika tumewaona na tumeanza kuwafanyia kazi ya kuwaangalia na kuwafuatilia naimani kuna mmoja atatuvutia zaidi na tutakubaliana kumleta hapa kwetu,”

“Ukiangalia mechi zetu anatumika, Phiri Moses anafanya vizuri kwenye nafasi hiyo lakini kiasili eneo ambalo amekuwa akicheza ni nyuma ya mshambuliaji, lazima tulete straika dirisha dogo la usajili,”alisema Mgunda ambaye ni kocha wa zamani wa Coastal Union ya Tanga.

“Kulingana na mazingira yalivyo wakati huu bado kuna nafasi ya kumtumia nahodha, John Bocco na Habibu Kyombo naimani wananafasi ya kutupa kitu bora kwenye kufunga kwani hawa wote ni wachezaji wa Simba,”aliongeza Mgunda ambaye malengo yake kwa sasa ni Simba kucheza nusufainali ya Afrika.

Taifa la Ghana ndilo analotikea winga wa Yanga Bernard Morisson, ambae aliichezea Simba msimu uliopita.

SOMA NA HII  KUMEKUCHA SIMBA....VYUMA VYA KAZI KUANZA KUSHUKA....MASTAA WATAKAOACHWA HAWA HAPA...