Home Uncategorized NYOTA ANAYEPIGIWA HESABU NA SIMBA ANA TUZO MOJA MKONONI HUYU HAPA MBUKINABE

NYOTA ANAYEPIGIWA HESABU NA SIMBA ANA TUZO MOJA MKONONI HUYU HAPA MBUKINABE


SOGNE Yacouba, nyota wa Asante Kotoko ya Ghana ambaye inaelezwa kuwa mkataba wake umemalizika ndani ya klabu hiyo hivyo yupo huru kujiunga na klabu yoyote kwa sasa na miongoni mwa klabu zinazotajwa ni Simba na Azam FC kwa Bongo kwamba zinahitaji saini yake.

Amezaliwa Januari 10, 1992 nchini Burkina Faso na nafasi anayocheza uwanjani ni mshambuliaji na ana tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Machi aliyopewa mwaka 2018 alipokuwa akiitumikia klabu yake ya Asante Kontoko.

2016 alikuwa akikipiga ndani ya Klabu ya Etoile de Ouagadougou ya Burkina Faso kabla ya kuibukia Ghana nyota mwenye miaka 28.

SOMA NA HII  MORRISON ATAJA SABABU YA KUTUA NDANI YA YANGA