Home Uncategorized SHEVA APEWA MAZOEZI MAALUMU, AWAOMBA MASHABIKI WAMUOMBEE

SHEVA APEWA MAZOEZI MAALUMU, AWAOMBA MASHABIKI WAMUOMBEE


MIRAJ Athuman ‘Sheva’ anatarajiwa kuanza mazoezi ya kunyonga baiskeli kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kurudi rasmi uwanjani akitokea kwenye majeraha.

 Sheva ameweka wazi kwamba mazoezi hayo ya wiki mbili yatamfanya arudi katika ubora wake uleule ambao alikuwa nao kabla ya kupata majeraha hayo. 

Sheva anatibu majeraha ya mfupa mdogo katika mguu wa kulia ambayo aliyapata akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na alitonesha tena majeraha hayo alipokuwa na Klabu ya Simba kwenye mchezo wa Fainali wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.


Sheva amesema: “Kwa sasa nimepewa mazoezi maalumu ambayo nitayafanya ili kurejea kwenye ubora wangu, kwa muda wa wiki mbili nitakuwa ninaendesha kibaskel maalumu kwa ajili ya kujiweka sawa, mashabiki waniombee,” .

Sheva ametupia mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara na ametoa pasi moja ya bao huku akisababisha penalti mbili zilizofungwa na mshambuliaji Meddie Kagere.

SOMA NA HII  PICHA YA TAWI LA SIMBA LA BANDARI KAVU-KWALA ILIYOZUA GUMZO HII HAPA