Home Uncategorized WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAPEWA KAZI MAALUMU

WACHEZAJI MTIBWA SUGAR WAPEWA KAZI MAALUMU

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa wachezaji wanapaswa watulie na familia zao na kutoa elimu kuhusu Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kwa sasa wamevunja kambi kufuatia agizo la Serikali.

“Tumevunja kambi kutokana na agizo la Serikali kutoruhusu mikusanyiko isiyo ya lazima ili kujikinga na kusambaa kwa Virusi vya Corona, tumewaambia wachezaji kwamba wanapaswa watulie na familia na kutoa elimu bora ya kujikinga na virusi kwani wao ni mabalozi.

“Kwa sasa hatutakuwa na kambi tumeivunja rasmi kila mchezaji ataendelea na ratiba zake akiwa nyumbani, ni matumaini yetu baada ya muda hali itatengamaa na maisha yataendelea,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA NA VICHEKESHO VIPYA KILA SIKU