Home Habari za michezo PANDA SHUKA YA BOCCO NA KAGERE YAMUIBUA METACHA…AFUNGUKA HALI JINSI ILIVYO WAKIKUTANA…

PANDA SHUKA YA BOCCO NA KAGERE YAMUIBUA METACHA…AFUNGUKA HALI JINSI ILIVYO WAKIKUTANA…


Kipa wa Polisi Tanzania, Metacha Mnata amedai si sahihi kuwabeza mastraika wa Simba, Meddie Kagere, Chris Mugalu na John Bocco kwani mpira hauko hivyo.

Metacha alisema licha ya kutoka suluhu dhidi ya Simba, hakuondoi ubora wa wachezaji hao, ambao msimu uliyoisha walifunga mabao, Bocco akiwa kinara wa mabao 16, Mugalu (mabao 15) na Kagere (mabao 14).

“Mashabiki watuulize sisi tunaokutana na washambuliaji hao uwanjani, kilichowapata ni upepo mbaya kwenye Ligi Kuu Bara, ndiyo maana mechi za CAF wanafanya vizuri,” alisema Metacha na kuongeza;

“Licha ya kutoka suluhu na sisi, naamini watapata matokeo kwenye mchezo wao wa CAF, ipo siku Kagere, Bocco na Mugalu watapewa heshima yao, binafsi nina imani nao kabisa.

“Wachezaji tunapitia vipindi vigumu, nawaelewa mastraika hao jinsi wanavyojisikia, ila wao siyo wa kwanza, wajipange zaidi ili miguu yao ije ijibu kwa matendo,” alisema.

Juma Makapu alisema “Siku mastraika wa Simba wakianza kufunga watakuwa wamewasha moto na itakuwa ngumu kuzimika, mchezaji akikosa kujiamini unadhani kaishiwa, lakini siku akirejea kwenye fomu ndipo utajua ubora wake.”

SOMA NA HII  SASA HAKUNA TENA MKEKA KUCHANIKA...FANYA HIVYI NA MERIDIANBET UKIONA MKEKA WAKO UNAUNGUA....