Home CAF STRAIKA HATARI WA ORLANDO AMBAYE ALITESA AFCON NA MALAWI…KAITUPIA SIMBA NENO HILI…

STRAIKA HATARI WA ORLANDO AMBAYE ALITESA AFCON NA MALAWI…KAITUPIA SIMBA NENO HILI…


WINGA wa Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini, Gabadinho Mhango, ametaja sababu kubwa inayowafanya Simba kupata matokeo mazuri katika michezo ya nyumbani inatokana na uwepo wa mashabiki wengi wanaowasapoti.

Gabadinho ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Malawi, ni moja kati ya wachezaji wenye majina makubwa ndani ya Orlando Pirates ambao April 17, mwaka huu wanatarajiwa kuwa wageni wa Simba katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Winga huyo amesema sababu kubwa ya Simba kufanya vizuri katika michezo ya nyumbani ni kutokana na wingi wa mashabiki wao ambao wamekuwa wakijitokeza mara kwa mara kuwasapoti jambo ambalo anaamini linaweza kuwa kikwazo kuelekea mchezo ujao.

“Sio kwamba ninafahamu sana kuhusu soka la Tanzania, lakini tayari tumeona vitu vingi kuhusu Simba na tunaifuatilia kwa kuwa ndio timu ambayo tutapambana nayo basi ilikuwa lazima kuangalia kuhusu nguvu yao ipo wapi.

“Kuhusu hofu juu yao pindi tunapokutana wakiwa nyumbani nadhani si sana japo mara nyingi katika michuano hii timu ambazo zimekuwa zinafanya vizuri ni zile zinazokuwa nyumbani, lakini tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo huo,” alisema winga huyo.

Simba katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, hadi sasa imecheza mechi nne nyumbani na kushinda zote.

Katika mchezo wa Jumapili hii, Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limeiruhusu Simba kuingiza mashabiki 60,000 ambao ndiyo idadi kamili wanaoingia Uwanja wa Mkapa. Awali waliruhusiwa kuingiza mashabiki 35,000.

SOMA NA HII  HIZI HAPA BILIONI 80 ZA MERIDIANBET ZINAKUNGOJA....KUSHINDA NI RAHISI MNOOOO....