Home Habari za michezo RASMI…’FEI TOTO’ NA AUCHO WAWEKWA CHINI YA ULINZI YANGA…ISHU NZIMA IKO HIVI...

RASMI…’FEI TOTO’ NA AUCHO WAWEKWA CHINI YA ULINZI YANGA…ISHU NZIMA IKO HIVI AISEE…


JOPO la madaktari wa Yanga chini ya Mtunisia, Youssef Ammar, umewaruhusu viungo wao, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Khalid Aucho kuanza mazoezi chini ya uangalizi maalum.

Viungo hao wote walikuwa nje ya uwanja kwa muda wa takribani wiki tatu wakisumbuliwa na maumivu ya misuli.

Akizungumza Ammar alisema Fei Toto alianza mazoezi mepesi Jumatatu ya wiki hii chini ya Kocha wa Viungo, Helmy Gueldich raia wa Tunisia.

Ammar alisema Fei Toto atamaliza mazoezi hayo wiki hii kabla ya wiki ijayo kuanza ya pamoja na wenzake sambamba na kuuchezea mpira.

“Fei Toto ana asilimia mia moja ya kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Simba, hii ni baada ya kupona maumivu yake ya misuli yaliyomuweka nje kwa muda.

“Anarejea uwanjani katika mchezo mkubwa na muhimu kwetu kupata ushindi utakaotuwezesha kupata pointi tatu na kuwa katika nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa wa ligi.

“Suala la kucheza au kutocheza lipo chini ya Kocha Mkuu Nabi (Nasreddine) ambaye ndiye anayeamua nani wa kucheza katika mechi husika kulingana na mikakati yake.

“Kuhusu hali ya Aucho, tayari nimemalizana naye, hivyo kwa sasa anajiunga na kocha wa viungo na anaweza kucheza mchezo unaofuata dhidi ya Simba,” alisema Ammar.

SOMA NA HII  ZORAN : NATAKA KUFIKA MBALI NA SIMBA....YANGA NAIJUA KIDOGO SANA...NINGEPEWA MIAKA MINNE INGEKUWA POA SANA...