Home kimataifa CITY YAPOTEZA MBELE YA TOTTENHAM

CITY YAPOTEZA MBELE YA TOTTENHAM


NUNO Espirito Santo, Kocha Mkuu wa Tottenham kikosi chake kwenye mchezo wa Ligi Kuu England kimewatikisa mabingwa  watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City baada ya timu hiyo kushinda kwa bao 1-0 na kusepa na pointi tatu mazima.

Ni bao la Heung-Min Son katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Tottenham Hotspurs na kushuhudiwa na mashabiki 58,262. Son alimaliza shughuli ya ushindi dakika ya 55 na kuwafanya mabingwa hao watetezi kupata mshutuko kwenye mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kwanza kwa timu hizo msimu mpya wa 2021/22.

Pep Guardiola, Kocha Mkuu wa City ambaye alimtumia kwa mara ya kwanza mchezaji wake mpya Jack Grealish amesema kuwa matokeo ambayo wameyapata ni mabaya kwa kuwa walihitaji ushindi hivyo wanahitaji muda zaidi ili kuweza kurejea kwenye ubora na kupata matokeo mazuri katika mechi zao zijazo.

Kwa upande wa Nuno ambaye mchezaji wake Japhet Tanganga alikuwa mchezaji bora wa mchezo licha ya kukosa huduma ya mshambuliaji wake Harry Kane amesema kuwa bado kuna mambo hayajatimia hivyo wana kazi ya kufanya kuwa imara zaidi.

SOMA NA HII  EPL, BUNDESLIGA NA LIGUE 1 KUENDELEA WIKENDI HII