KLABU ya Chelsea imesepa na pointi tatu mazima mbelw ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Stamford Bridge.
Baada ya dakika 90 kukamilika ilikuwa Chelsea 3-0 Crystal Palace. Ni Marcos Alonso dk 27, Christian Pulisic dk 40 na Trevoh Chalobad dk 58 walipachika mabao hayo.
Chelsea ilipiga jumma ya pasi 678 huku Crystal Palace ikipiga jumla ya pasi 423. Kwa upande wa mashuti ambayo yalilenga lango ni 6 kwa Chelsea na moja kwa upande wa Crystal Palace.