Home Simba SC GOMES AKOMALIA WACHEZAJI WAKE KUTUPIA, KAMBI MOROCCO IMEPAMBA MOTO

GOMES AKOMALIA WACHEZAJI WAKE KUTUPIA, KAMBI MOROCCO IMEPAMBA MOTO


 KOCHA wa Simba, Didier Gomes, amesema kuwa moja kati ya programu ambayo anaitilia mkazo kwa sasa akiwa Morocco ni wachezaji wake kufunga mabao ya mbali.


Gomes alisema kuna kazi 
nyingi za kufanya akiwa Morocco, lakini kubwa zaidi ni timu kuweza kufunga kwa kila namna ikiwemo nje ya boksi la wapinzani kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na njia nyingi za kupata ushindi wakati wa mechi.


Simba kwa sasa ipo Morocco ilipoweka kambi ya kujiandaa na msimu wa 2021/22 ambapo ipo huko tangu Jumatano wiki hii.


Akizungumzia maendeleo ya kambi hiyo, Gomes alisema kila kitu kinakwenda vizuri kutokana na mazingira yalivyo na kwa sasa wanaangalia namna nzuri ya timu kutimiza kila program waliyoiweka.


“Kambi ipo vizuri kutokana na nchi ambayo tupo hali ya hewa yake kuwa nzuri kwetu, kambi hii ina faida nyingi kwa sasa, tunaagalia zaidi wachezaji kufunga nje ya boksi, tunajaribu kuangalia namna gani vijana watafanyia kazi eneo hilo kwa sasa,” alisema Gomes.


Simba ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara walilotwaa msimu wa 2020/21 baada ya kufunga mabao 78 na kufikisha jumla ya pointi 83.


Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kambi hiyo ni pamoja na kiungo Jonas Mkude na mshikaji wake Taddeo Lwanga, Bernard Morrison, Meddie Kagere, Erasto Nyoni na Hassan Dilunga.

SOMA NA HII  MANARA:- AHMED ALLY NI YANGA 'LIA LIA' ANAYESAKA UGALI SIMBA...HATA MIMI NILIKUWA HIVYO...