Home Habari za michezo MANARA:- AHMED ALLY NI YANGA ‘LIA LIA’ ANAYESAKA UGALI SIMBA…HATA MIMI NILIKUWA...

MANARA:- AHMED ALLY NI YANGA ‘LIA LIA’ ANAYESAKA UGALI SIMBA…HATA MIMI NILIKUWA HIVYO…

Habari za Michezo

“Nakiri kwamba hata mimi wakati najitafuta, niliibukia kuwa Mfuasi feki wa Madunduka, na ilifika mahali nikawa nawacharura mno Yanga hadi mimi mwenyewe ilikuwa inanikera, lakini ndio kujitafuta huko, ningefanyaje ndugu zangu? Na bila kufanya hivyo GSM wangenionaje ? Ile Siku waliyoniambia rudi home sasa, ooohh ilikuwa siku kubwa sana kwangu, SITASAHAU

Basi bhana Wakulungwa, ndio story ya huyu kijana mkazi wa Tambuka Reli, kelele na kebehi zote anazosema dhidi yetu,ichukuliwe ni kwenye kujitafuta na kujipapatua tu, huyu anaumwa na Yanga yake, hali hata Chakula siku Wananchi wakiwa wanacheza, Kigosi @raythegreatest na @jimmymafufu waliwahi kuniambia walikuwa wanampa hadi hirizi kuvaa,siku ya mechi ya Yanga

Miaka ya nyuma ilikuwa kila asubuhi anaenda Jangwani kubusu na kupiga picha na Makombe yetu, na akifika tu anaamkia, Shkamoo Makombe na Wazee wetu pale klabuni walikuwa wanampenda kwa ule usafi wake wa kusafisha kila siku Makombe yetu, hadi Jiki alikuwa anayaoshea.

Kwa hiyo msameheni Wanayanga, anajitafuta tu,ni kijana wetu mzuri na ana msaada mkubwa kwetu, Mtu wa maana sana na ni familia kabisa, Soon Mtanielewa Wananchi”

Ameandika @hajismanara

SOMA NA HII  WAWA AVUNJA UKIMYA SIMBA...AANIKA WAZI MAHUSIANO YAKE NA PABLO..ATAJA TOFAUTI ZAO..