Home Simba SC ISHU YA LUIS KUIBUKIA YANGA MANARA AFUNGUKA

ISHU YA LUIS KUIBUKIA YANGA MANARA AFUNGUKA


 WAKATI tetesi zikieleza kuwa kiungo wao fundi wa kutumia mguu wa kushoto kufunga Luis Miquissone yupo kwenye rada za Yanga uongozi wa Simba umesema kuwa bado dili hilo halijakamilika na mkwanja unaohitajika ni mrefu.

Ndani ya ligi, Luis akiwa ametupia mabao 9 amefunga mabao 7 kwa mguu wa kushoto huku moja akitumia mguu wa kulia na lingine alifunga kwa kichwa dk 90 mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.

Haji Manara Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa hakuna taarifa yoyote kuhusu mchezaji huyo kuuzwa na badala yake timu itakayomhitaji lazima itoe mkwanja mrefu kupata saini yake.

“Hakuna ambaye anaweza kusema kwamba mchezaji wa Simba ni mali yao kwa sasa, hakuna tetesi za namna hiyo eti unasema mchezaji anatakiwa na timu fulani wakati bado ana mkataba?

“Kuna mob ambayo inapenda kwenda na mambo hasa yanapotokea na tunayajua ila sio kwa hili hakuna jambo kama hilo, Simba tupo tofauti kabisa, ikiwa kuna timu kutoka Tanzania inamuhitaji Luis ijiandae kutoa dola milioni 10,” amesema.

Mbali na abao 9 ambayo amefunga kwenye ligi pia Luis ametoa jumla ya pasi 10 za mabao kwa msiu wa 2020/21.

SOMA NA HII  PAMOJA NA BARBARA KUTIMKA SIMBA....HAYA HAPA MAMBO MAZITO ALIYOYAFANYA KWA MIAKA MIWILI TU.....