Home Uncategorized KANE AFIKISHA MABAO 200

KANE AFIKISHA MABAO 200


 NYOTA wa Klabu ya Tottenham Hotspur Harry Kane ameweka rekodi ya kufikisha jumla ya mabao 200 klabuni hapo.


Kane alifikisha idadi hiyo baada ya kufunga bao 1 kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ludogorets kwenye Ligi ya Europa, Novemba 5.


Anakuwa ni mchezaji wa tatu kufikisha idadi ya mabao hayo ndani ya Spurs akiwa nyuma ya Bobby Smith mwenye mabao 208 na Jimmy Greaves mwenye mabao 266.


Kane ametupia jumla yamabao 12 kwenye michuano yote na ametoa jumla ya asisti 10.

SOMA NA HII  HII HAPA TIMU AMBAYO NYOTA GUSTAVO WA BRAZIL ALICHEZA MECHI NYINGI