Home Habari za michezo BAADA MAWIMBI MEENGI KUIPIGA SIMBA MSIMU HUU…DEWJI ARUDISHA MAJESHI RASMI SIMBA…TRY AGAIN...

BAADA MAWIMBI MEENGI KUIPIGA SIMBA MSIMU HUU…DEWJI ARUDISHA MAJESHI RASMI SIMBA…TRY AGAIN AINJINIA KILA KITU…


AWALI kulikuwa na tofauti kati ya Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi Simba, Kassim Dewji na viongozi wengine wa ngazi ya juu kwenye klabu hiyo.

Viongozi wa juu wa Simba walikuwa na maelewano si ya kulizisha na Dewji ambaye alikuwa pembeni ya timu tangu mwezi Desemba mwaka jana.

Baada ya Dewji kuwa nje ya timu kutokana na maelewano yasikuwa ya kulizisha hakufanya jambo lolote kwa timu na aliamua kukaa pembeni na kuangalia tu kinachoondelea kwenye klabu na uongozi.

Mapema mabosi hao wamekutana leo na kufanya kikao kizito kisha kumaliza tofauti zao za hapo awali hadi kushindwa kuwa na maelewano mazuri.

Dewji kabla ya kuondoka kwenye uongozi alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba na alisimamia usajili wa dirisha dogo msimu huu.

Baada ya kumaliza kikao hicho na tofauti zao kuisha Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ atampangia majukumu kama ni yale yale ya awali au atabaki kwenye uongozi tu.

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUKIRI KUTUMA MAOMBI YA KUMSAJILI CHAMA...SIMBA WATIA NGUMU..