Home Habari za michezo SASA NI RASMI…GEORGE MPOLE KACHUKUA MIKOBA YA JOHN BOCCO…MCHEZO MZIMA ULIKUWA HIVI…

SASA NI RASMI…GEORGE MPOLE KACHUKUA MIKOBA YA JOHN BOCCO…MCHEZO MZIMA ULIKUWA HIVI…


MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, George Mpole ameibuka kinara wa ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22, baada ya kufikisha mabao 17 na kumpiku nyota wa Yanga, Fiston Mayele aliyemaliza na mabao 16.

Kabla ya mchezo wa leo wa kuhitimisha msimu nyota hao kila mmoja alikuwa na mabao 16 huku akisubiriwa ni nani ataibuka kidedea katika michezo hii ya mwisho.

Mpole alifunga bao lake la ushindi dakika 11 ya mchezo wakati timu yake ikitoka sare ya 1-1 na Coastal Union katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Geita Gold ilikuwa ya kwanza kupata bao hilo kabla ya Rashid Chambo kuisawazishia Coastal Union dakika ya 19 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare na kumwachia Mpole kushinda kinyang’anyiro hicho baada ya Mayele kushindwa kufunga dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mpole kwa sasa anavuka rekodi ya mshambuliaji wa Simba, John Bocco aliyemaliza kinara wa ufungaji bora msimu uliopita wa 2020/2021 akifunga mabao 16.

Matokeo haya yanaifanya Coastal Union kumaliza msimu ikiwa nafasi ya saba na pointi 38 huku Geita Gold ikimaliza ya nne na pointi 46.

SOMA NA HII  SAMATA AKAMATIKI TENA REKODI ZAKE NI ZAIDI YA HISTORIA