Home Azam FC KOCHA ‘MMOROCCO’ KUONDOKA NA UBINGWA WA YANGA MSIMU HUU….

KOCHA ‘MMOROCCO’ KUONDOKA NA UBINGWA WA YANGA MSIMU HUU….

Habari za Yanga leo

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Rachid Taoussi amesema kama kila mchezaji atajitoa kwa asilimia 80 ana uhakika wa ubingwa msimu huu.

Akizungumza na kunukiliwa na gazeti la  SpotiLEO, kocha huyo raia wa Morocco amesema pamoja na ugumu uliopo kwenye ligi lakini amegundua kwamba baadhi ya wachezaji wake wamepoteza ari ya kupambana jambo ambalo limechangia kutopata ushindi katika baadhi ya mechi.

“Hatutakiwi kuzitolea macho mechi za Simba na Yanga ari yetu inatakiwa kuwa juu ndivyo wanavyofanya wenzetu na baada ya kulibaini hilo nimezungumza na wachezaji nikitaka kila mmoja ajitoe angalau kwa asilimia 80 ili kubeba ubingwa mwishoni mwa msimu huu,” amesema Taoussi.

Kocha huyo amesema siri kubwa ya mafanikio ya timu za Simba na Yanga ni wachezaji wao kucheza kwa kujituma na ari kubwa ya mapambano katika mechi zote za ligi kitu ambacho msimu huu anataka kukiona kwa wachezaji wake.

Taoussi ameongeza kuwa ingawa hawajaanza vizuri msimu ukilinganisha na timu hizo mbili lakini bado hawajachelewa wana nafasi ya kurekebisha makosa yao na kuibuka mabingwa msimu huu.

Kwa sasa Azam FC inakamata nafasi ta tatu kwenye ligi ikiwa na pointi 15 baada ya kushuka dimbani mara nane, watashuka tena uwanjani Oktoba 29 wakiikaribisha Ken Gold kwenye Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  SIMBA WASIPOBADILIKA HAPA WATAENDELEA KUFA KIUME KWENYE ROBO FAINAL ZA CAF...