Home Habari za Yanga Leo GAMONDI AWAPA PROGRAMU MAALUM MASTAA WAKE…YMO AZIZ KI NA PACOME

GAMONDI AWAPA PROGRAMU MAALUM MASTAA WAKE…YMO AZIZ KI NA PACOME

Habari za Yanga leo

MUITE Miguel Gamondi Master, Hataki masihara na chama lake, amewapatia programu maalum mastaa wake, ili kuwafanya wawe timamu kimwili na akili pindi msimu mpya wa ligi utakaporejea.

Gamondi amesambaza programu, kulingana na kile walichokifanya wachezaji msimu ulioisha, wapo ambao watachukua muda mrefu katika mapumziko na wale ambao watatakiwa wafanye kazi ya ziada kujiweka fiti, ili msimu mpya utakapoanza wawe na uwiano wa kuonyesha kiwango bora.

Katika mazungumzo yake na Mwanaspoti, alitolea mfano wa Attoula Yao jinsi ambavyo alitumika sana msimu ulioisha, kwamba anastahili mapumziko ya kutosha ili kuupa mwili wake nguvu.

“Kuna wachezaji ambao walicheza dakika nyingi, ili kuepusha miili yao isipate fatiki inawalazimu kuipumzisha miili yao, ili watakaporejea wawe na nguvu mpya, kuna kina Yao, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya,Dickson Job, Maxi Nzengeli na Djigui Diarra.

Aliongeza “Ukiachana hao, kuna wale ambao walipata na majeraha wakati Ligi Kuu inaisha hawakuwa na ufiti kama Khalid Aucho, Pacome Zouzou, hao nao programu yao ipo tofauti, wanakwenda kutafuta ufiti wa kujiweka sawa.

“Ukiacha hao wapo wale ambao walikuwa hawapati nafasi kubwa ya kucheza, nao watapaswa kupambana ili wakirejea wawe tayari kwa kutumika, maana utakuwa msimu wa kazi tu.”

Akizungumzia usajili unaoendelea amesema amekabidhi ripoti kwa viongozi wao ndio wanaofanyia kazi suala hilo la kusajili lakini anafuraha kuona wachezaji wake wote muhimu wameendelea kubaki ndani ya timu hiyo.

“Kazi yangu nimeikamilisha ni kuhakikisha nakabidhi ripoti haraka ili iweze kufanyiwa kazi hilo nimewaachia viongozi ambao tayari wamenihakikishia kubakiza mastaa wangu wote walionifanyia kazi nzuri msimu ulioisha,”

Aliongeza kuwa; “Endapo wataniongezea na wachezaji wa nafasi nilizopendekeza zifanyiwe kazi basi natarajia kuwa na msimu mwingine bora na naamini wachezaji hawataniangusha kuweza kufikia malengo,”alisema Gamondi.

SOMA NA HII  MPAKA KUFIKIA 'RAUNDI' KWENYE LIGI...YANGA NDIO MWAMBA KWENYE KILA KITU...TAKWIMU HIZI HAPA..