Home Uncategorized WAYNE ROONEY ALIKUWA ANAIFIKIRIA BARCELONA

WAYNE ROONEY ALIKUWA ANAIFIKIRIA BARCELONA


NYOTA wa zamani wa Klabu ya Manchester United, Wayne Rooney ameweka wazi kuwa alikuwa anapenda kujiunga na Klabu ya Barcelona zama zile iliporipotiwa kwamba anahitaji kuondoka ndani ya kikosi hicho.


Msimu wa 2010 wakati akiwa ndani ya Manchester United ilielezwa kuwa nyota huyo anahitaji kuondoka ndani ya Manchester United ili apate changamoto mpya baada ya kujiunga na timu hiyo msimu wa 2004 akitokea Klabu ya Everton.

Ndani ya Manchester United aliyodumu mpaka msimu wa 2017 alicheza jumla ya mechi 393 na kufunga mabao 183 na alirejea tena kwenye timu yake ya zamani ya Everton msimu wa 2017-18 ambapo aliweza kuja kwenye ardhi ya Tanzania kwenye fainali ya Kombe la Sport Pesa walipocheza na Klabu ya Gormahi.

Rooney alitaka kuondoka ndani ya Old Trafford ambapo alitaka kupata changamoto mpya ameweka wazi kuwa alikuwa anafikiria kucheza ndani ya Barcelona ile iliyokuwa na Lionel Messi nchini Hispania baada ya kucheza kwa muda mrefu Ligi Kuu ya England.

“Kutoka ndani ya moyo wangu nilikuwa ninapenda kuondoka na kujiunga ndani ya Hispnia, kiukweli nilikuwa ninapenda kwenda Barcelona zaidi kuliko ndani ya Real Madrid isingekuwa hivyo labda ningekwenda hata Chelsea ningefurahi.

“Nakumbuka niliwahi kukaa chini nikafikiria kwamba ingekuaje ningecheza timu moja na Messi, Xavi, Iniesta na Busquets, na zama zile Messi hakuwa  anacheza kama anavyocheza sasa kama namba 9,” amesema.

SOMA NA HII  ZAHERA ATAJA HATMA YA YONDANI NDANI YA YANGA