Home Habari za michezo AFL KUTIMUA VUMBI MWEZI HUU WABABE HAWA KUKUTANA

AFL KUTIMUA VUMBI MWEZI HUU WABABE HAWA KUKUTANA

WACHEZAJI MAMELODI WASHIKWA NA NJAA…TUOMBE WASIKUTANE NA SIMBA SC

Baada ya Simba, TP Mazembe, Enyimba na Petro de Luanda kutolewa kwenye michuano mipya ya African Football League, Juzi vigogo wanne waliobaki walicheza mechi mbili za nusu fainali za kwanza ambazo zilikuwa za moto.

Al Alhy iliyoitoa Simba kwa sheria ya bao la ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa 3-3, juzi ikiwa ugenini Afrika Kusini, ilikubali kichapo cha bao 1-0, kutoka kwa Mamelodi Sundowns bao lililofungwa na Thapelo Maseko dakika ya 52 ya mtanange huo.

Wababe wa TP Mazembe, Esperance de Tunis, nao walijikuta wakiangukia pua ugenini Morocco, baada ya kuchapwa bao 1-0, na Wydad AC ambao waliiondosha Enyimba. Bao hilo lilifungwa na Hicham Boussefiane dakika ya 58.

Hata hivyo bado haijaisha kwani hizo zilikuwa mechi za mkondo wa kwanza ambapo timu zote zilizopoteza zilikuwa ugenini na nusu fainali za pili zitakuwa nyumbwani jambo linaloongeza ushindani wa michuano hiyo.

Mechi hizo za marudiano zitapigwa kesho, Novemba mosi, ambapo Al Ahly itakuwa nyumbani Cairo, kuikaribisha Mamelodi huku Esperance itakuwa maskani kwake, Tunis, kuikaribisha Wydad.

Baada ya mechi hizo, washindi wa jumla watatinga fainali ambayo pia itapigwa nyumbani na ugenini na mchezo wa kwanza utakuwa Novemba 5, huku marudiano yatakuwa Novemba 11, na hapo ndipo bingwa wa kwanza katika michuano hiyo atapatikana.

Katika msimu wake wa kwanza, mashindano hayo yamehusisha timu nane pekee lakini inatarajiwa kuanzia msimu wa pili zishiriki timu 22.

SOMA NA HII  KUMEKUCHA SIMBA...ACHANA NA MANZOKI...STRAIKA HILI LA MABAO LANUKIA MSIMBAZI...