Home Uncategorized ZAHERA ATAJA HATMA YA YONDANI NDANI YA YANGA

ZAHERA ATAJA HATMA YA YONDANI NDANI YA YANGA



KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa beki wa kikosi hicho Kelvin Yondan hawezi kugoma kama ambavyo inadaiwa hivyo atajiunga ndani ya kikosi hicho muda wowote.


Kelvin Yondani ni mchezaji pia wa timu ya Taifa ni miongoni mwa wachezaji ambao hawajijiunga na timu kambini Morogoro kwa madai ya kuigomea Yanga kushinikiza kulipwa stahiki zao.

Wachezaji wengine ambao hawajajiunga na kambi ni pamoja na Juma Abdul na Andrew Vincet ‘Dante’.

Zahera amesema: “Yondani hawezi kugoma ndani ya Yanga kwani ninachojua mimi yeye alipewa likizo na anatumikia pia timu ya Taifa hivyo baada ya majukumu yake atarejea ndani ya kikosi cha Yanga,”amesema.

Zahera ameshawasili kambini Morogoro na jana alishuhudia mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Mawenzi Market uwanja wa Jamhuri na waliibuka kidedea kwa bao 1-0.
SOMA NA HII  DODOMA FC YAUNGANA NA GWAMBINA FC MSIMU WA 2020/21 ZIPO NDANI YA LIGI KUU BARA