Home Uncategorized KOCHA STARS ATAJA KILICHOWAZUIA KUPATA USHINDI MBELE YA KENYA

KOCHA STARS ATAJA KILICHOWAZUIA KUPATA USHINDI MBELE YA KENYA

ETTIENE Ndayiragije, Kaimu Kocha wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amesema kuwa sare waliyoipata imetokana na kushindwa kutumia nafasi walizozipata hivyo ni muda wa kufanyia kazi makosa waliyoyafanya.

Stars jana ilikubali suluhu ya bila kufungana na timu ya Taifa ya Kenya kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu michuano ya Chan itakayofanyika Cameroon mwaka 2020.

“Wachezaji wamejituma na wamefanya kazi kwa juhudi, kilichoshindikana ni kutumia nafasi ambazo wamezipata hivyo ni wakati wetu kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marudio nchini Kenya.

“Sapoti ya mashabiki ina nguvu nasi pia tunajipanga upya kwani kwenye mchezo yote ni matokeo licha ya kutokuwa na mpango wa kupata sare,” amesema. 

Stars itamenyana na Kenya mchezo wa marudio kati ya Agsti 4 nchini Kenya.

SOMA NA HII  MWILI WAFUKULIWA, WAVULIWA SARE ZA KAZI