Home Habari za michezo KWA MARA YA KWANZA ..SIMBA WAVUTISHWA PUMZI YA MOTO CHINI YA KOCHA...

KWA MARA YA KWANZA ..SIMBA WAVUTISHWA PUMZI YA MOTO CHINI YA KOCHA MPYA…WAARABU KAMA KAWA WAMEJIPIGIA..


Wekundu wa Msimbazi Simba SC wamekubali kichapo cha bao 2-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Haras El Hadoud ambayo imepanda daraja na itacheza Ligi Kuu ya Misri msimu ujao.

Mchezo huo ambao ni wa tatu wa kirafiki, ndio wa kwanza kwa wekundu hao kupoteza wakiwa kambini katika mji wa Ismailia nchini Misri baada ya kushinda mchezo mmoja na mwingine sare ya 1-1.

Magoli hayo ya Haras yalipatikana dakika ya 2 ya mchezo kwa penalti na linguine dakika ya 55 ya mchezo ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Kikosi kilichoanza kwenye mchezo huo kilikuwa na Beno Kakolanya, Israel Patrick, Gadiel Michael, Joash Onyango, Henock Inonga, Jonas Mkude, Peter Banda, Clatous Chama, Moses Phiri, Pape Sakho na Augustine Okrah.

SOMA NA HII  YANGA WATAMBA KUONGEZA MAKALI YA FISTON MAYELE, MAKAMBO